[Page principale | Evangile | Cantiques en français | Commentaires et explications sur la Bible | La Bible]
Nyimbo Swahili
1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 16, 17, 18, 19, 20, 21, 22, 23, 24, 25,
26, 27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 41, 42, 43, 44, 45, 46, 47, 48, 49, 50,
51, 52, 53, 54, 55, 56, 57, 58, 59, 60, 61, 62, 63, 64, 65, 66, 67, 68, 69, 70, 71, 72, 73, 74, 75,
76, 77, 78, 79, 80, 81, 82, 83, 84, 85,
Tunakuabudu Baba Mungu
Wewe uishie nuruni
Unapambanua mbingu
Twakusanyika mbele yako
Wana wa pendo lako kubwa
Tunasifu jina lako,
{Tunakuheshimu,
Muumba wa vyote
Aleluya ! utukufu,
Kwake Mungu na Mwokozi
Aleluya !}
Wewe ulituangazia,
Mwenye enzi, Baba wa neema,
Kupitia Mwana wako
Kwake tunakubariki,
Twakuabudu, tunakusifu
Na kukutukuza hapa,
{Tunakuheshimu,} etc.
Tuimbe wimbo takatifu
Wakusifu Mwana wa pekee,
Milele Mwana wa Mungu
Kwa kufa na kuishi kwake
Alifunua neema kubwa
Njia nzuri ya mbinguni
Sifa na heshima
Kwa yesu Mwokozi
Aleluya ! utukufu,
Kwako Bwana !
Aleluya! Aleluya.
Yesu tunakuheshimu
Utakayebaki milele
Wimbo wa wakombolewa.
Uliumizwa tuokoke
Ulichubuliwa tupone
Tuishi kwa ufufuko
Sifa na heshima
Kwa Yesu Mwokozi etc.
Yesu ukombozi wetu
Kwa teso ulitupatia
Ukombozi wa milele
Bwana mwenye utukufu
Ndani yako tuna amani,
Na ushindi na baraka.
Mwokozi muzuri
Uketiye juu
Kwa uzuri
Na heshima
Twakuabudu
Tutakukuza milele.
Tukuzwa Baba wetu (x2)
Uliyetuandalia makao juu mbinguni
Umetowa wokovu (x2)
Wastahili shukrani ya mapendo na kusifu
Tukuzwa Mwana Kondoo (x2)
Kwakuokowa kundi ulikufa msalabani
Ukashinda shetani (x2)
Mukombozi wa ajabu sifa ni kwako milele.
Kweli tukuzwa Bwana (x2)
Pokea pekee nguvu, kuzo, heshima na, ufalme.
Milele na milele (x2)
Tutaimba wokovu, ushindi wa wema wako.
Tukuze Mungu wa mapendo
Wa amani kwa wimbo safi
Aliye kwa wema fahari
funguwa njia ya mbingu
Kwa neema iliyo bora
Na sisi wabarikiwa,
Hai kwa moyo wa furaha
Tuinuwe nyimbo zetu.
Mioyo yetu yakutukuza
Mwenye uwezo na pendo
Sisi tunakutegemea
Kwa sasa na kwa milele.
Nguvu, wema, neema, uwezo
Ndani yako vinasifu
Na kanisa kwa uhakika
Lakungojea urudi.
Kwa Yesu tunatoa
Zabihu za sifa zetu
Kwa Yesu tunaabudu
Malaika vilevile
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika
Tulikuwa zambini
Sote wana wa gazabu
Ukatuweka huru
Ndani yako tuna Baba
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika
Na tumepewa Yesu
Na umetuweka kwake
Ndani yake tuliitwa
Kupewa taji milele
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.
Alituahidiya
Mwana aja kututwaa
Kwenye makao ya juu
Tupendapo kumungoja
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.
Hivi tutakukuza
Katika kuzo na nuru
Na tutasema tena
Na Kanisa lako lote
Mungu ubarikiwe tunapokusanyika.
Asifiwe Mwokozi
Na Mwana pekee wa Mungu
Alikuja duniani,
Kuokoa wenye zambi
Ee Yesu utukuzwe milele na milele, (x2).
Ee Mwana ulikuja
Kufa kifo cha aibu
Ukashinda kaburi
Kwa uwezo wa milele
Na Ulivunja nguvu za giza na mauti, (x2).
Kwa pendo ulikunywa
Kikambekichungu sana
Na ukatupatia
Kikombe cha ukombozi
Ee yesu utukuzwe milele na milele, (x2).
Sifa kwa Mwana Kondoo Mwokozi
Ndani yake kifo kilishindwa
Adui aliona nguvu yake
Vilevile kaburi inamutii
Utukufu kwako Yesu
Utukufu Bwana Yesu
Na kuzimu kumeshindwa
Ushindi (x2).
Vile Kristo alikataliwa
Na kukaa mbinguni akingaa
Na Kanisa lisilo julikana
Karibuni litavikwa utukufu
Utukufu kwako Yesu
Utukufu Bwana Yesu
Na kuzimu kumeshindwa
Ushindi (x2).
Yesu uliahidi kurudi
Kututafuta punde yu waja
Na wafalme katika utukufu
Tutaimba sote wimbo wa ushindi
Utukufu kwako Yesu
Utukufu Bwana Yesu
Na mauti imeshindwa
Ushindi (x2).
Kwa aliye tuokoa
Kwa damukatusafisha
ufalme na ukuu ni vyake
MwanaKondoo astahili
utajiri, heshima, nguvu,
mamlaka, hekima, na sifa (x2)
Kungaa kwa Sura kamili ya Mungu
Mwana wa milele muabudiwa
Sifa kwako wewe ustahiliye
Kuheshimiwa na wote milele.
Ulishuka ili uwe zabihu,
Kwako tu Mungu akatukuzwa
Utakatifu, upendo, haki yake
Msalaba ukavikuza vyote.
Sasa umeinuliwa kwa Mungu
Karibu na ukubwa mbinguni
Twakuona na utukufu mwingi
Mwana wa watu uliyefufuka.
Twakuabudu wewe ambaye taji
Lakumbusha mateso ya kifo
Bwana Yesu tutakusifu wewe
Tukikizunguka kiti cha enzi
Watoa neema na kuzo
E Bwana Mungu wetu, katika Yesu !
Ubarikiwe na wateule wako
Wenye uheri kukuamini (x2).
Ulitupatia neema,
iliyotupa usalama moyoni :
Wenye heri tutaingia mbinguni
Kunapongaa uso wako (x2).
Wewe watuwekea sifa
Iliyo ya MwanaKondoo mbinguni
Tutakuwa naye katika uheri,
tunda la kazi ya msalaba (x2).
Mungu wa neema na sifa !
Wapendwa wako wanaye Roho wako,
Kwa jina la Yesu tunakuabudu
Yeye ni ukombozi wetu (x2)
kukuimbia Mungu, wa mapendo na kweli
kuabudu, kubariki na kufurahi
kushangilia ushindi wa Bwana Yesu
Ni sehemu tuliyoitwaa kwa imani.
Jina lako lisifiwe, Neema yako
Iliyotujia katika uzuri
Tulikuwa gizani sasa uso wako
Waleta mishale ya nuru mioyoni.
Tupo wana wako, jina nzuri la Baba
Latujaza heri, hakika, amani
Roho wako mhuri, mwangaza na Mwalimu
Na karibu nawe tumekubaliwa.
Ni mapendo yako, kifo, uhai wako
Vilivyotuletea hii sehemu
Kila moja wetu asisahau kamwe
Kwamba tulitakaswa ili tumukuze.
Ukamilifu usiyoweza kusemwa
Wa uwezo, mapendo, hakibasiyokwisha, isiyokwisha
Mwana wa Mungu milele !
Utukufu wa mbinguni
Kwa amani yako, Kanisa lako pe ndwa
Lainama kuabudu (ter)
Wakaa ee Yesu, kwa kuume kwa Baba
Ukivikwa uwezo, nuru, utukufu na utukufu
Mungu wetu (x2)
Mioyo zetu (x2)
Yainama mbele yako kwa kutii
Pia kukuinua (ter).
Mbinguni kwa kiti cha Baba
Twakuona ee Mwokozi
Pumzikoni vile nuruni
Una uwezo na kungaa
Kazi ya neema imekwisha:
Umekaa patakatifu ;
Juu utukufu umepewa
Watawala juu ya vyote.
Twashinda kwa ushindi wako
Yesu Mwokozi muweza,
Juu katika utukufu
Umetangulia wako !
Tuna tumaini la mbingu,
Linalokutegemea
Tuna uhakika wa roho
Ni Musingi wa imani.
Sifa kwa kichwa cha kanisa!
Bibi arusi mupendwa
Pande zako punde atakaa,
Akibariki milele
Wewe Bwana mwenye uzuri
Tutakaofurahia,
Na pendo lako la ajabu
Litakuwa siku zote.
Mungu wa pendo na neema!
Twafurahi kukutana
Mbele ya uso wako mzuri
Kuabudu na kubariki
Na Katika salama yako
Kweli Upewe ibada,
Iletayo mashukurani,
Marashi : jina la Yesu.
Bwana ingia nafsi zetu
Na wema wako wa ajabu,
Utuwashie moto wako
Wa pendo lako Ee Bwana ;
Ndipo sifa zitatokea
Mioyoni mwetu kwa Roho
Ili tuimbe rehema zako
Na pendo ndani ya Yesu.
Tunapenda kuketi pale
Twawekwa na kazi yake
Na tunafuata nyayo zake,
Hadi mbinguni alipo
Ni pahali patakatifu
Ambapo mlango ni wazi
Sifa za waamini zapanda
Kwako kupitia Yesu
Umoja wa Kanisa wapendeza
Bwana Yesu, wakufurahisha
Kwa kulipenda ulijitolea
Wataka liwe nawe mbinguni
Roho yako Yesu yatukusanya
Karibu nawe katika pendo
Heri gani kukuabudu pamoja
Twatangaza kufa na kurudi
Ni kutamu ndugu wakikuabudu
Roho wako akiwa kiongozi
Katika nyimbo na maombi yetu
Tunayokutolea pamoja.
Ni kweli palipo uwepo wako
ukileta uhuru moyoni
kila mwamini katika amani
asikia nguvu, uhakika.
Na Itakuwaje kwa mukutano
Mbinguni kanisa litakuona
Furaha gani isiyo na mwisho
utukufuni likikuabudu.
Ulitualika, tena kwa siku hii
Mwokozi Muabudiwa ili tulishwe
Katikati ya jangwa, wajenga meza hii
Kumbusho la pendo lako (x2).
Kando yako, Bwana,kanisa lazunguka
Kukumbusha kifo chako hadi urudi,
Twavunja mukate, tunakunywa kikombe,
Kumbusho la pendo lako (x2)
Uovu wetu ulikulemea kichwani
Mzigo wa uchungu na muzito sana;
Lakini kwa amani, tunasherekea
Kumbusho la pendo lako (x2)
Tukionja mkate huu, na kinywaji hiki
Vinaelekeza macho yetu juu.
Na Punde tutamaliza safari yetu
Tutatambua u pendo (x2)
Asante Yesu, Mwokozi na Mwaminifu!
Bila kivli tutakuona mbinguni
Na tutatukuza, kwa sifa ya milele,
Ukubwa wa pendo lako (x2)
Mbele ya kiti cha baba
Akaapo kwa heshima
Jicho letu latazama
Uzuri wako Bwana
Utukufu ulio nao
Ndani ya kungaa kwako
Watuangazia kweli ndani ya mioyo yetu
Kungaa kwa uso wako
Siko kuvutiapo tu
Kwani neema yako kubwa
Yaangaa usoni mwako
Kwa neema ulishuka
Duniani mwa uasi
Ulipotuchukulia maovu hata zambi
Nafsi yashangaa sana
Juu ya upendo huu
Ulio mukubwa sana
Hauna hata mpaka
Hivyo sisi twatamani
Kurudi kwako hapa
Ili tuone, tutamke
Makuu ya pendo lako.
Tukaribie na kwa nyimbo zetu
Mwana Kondoo mupendwa akuzwe
Alishinda na alifufuka
Tutangaze makuu yake yote
Sisi wenye : kupendwa na Kristo (x2)
Alitufilia kama sadaka
Tukapokea upendo wake
Kwa kutuokoa katika giza
Alikubali fimbo za uhaki
Akafanywa : chukizo, laana (x2)
Twakuabudu sadaka ya toleo
Wewe ulitununua sisi
Tukumbushapo kifo, mateso
Tunangoja siku yakuonekana
Mbinguni : kama bibi arusi (x2).
Tunasherekea kwa meza hii
Pendo la Kondoo uliyechinjwa
Kwako roho zetu zinalindwa
Zikionja salama na uheri
Na kwa bei ulivinunua : ulivinunua (x2).
Mbele ya kiti cha neema
Twakuabudu Mungu wetu
Tukiingia patakatifu
Kwa njia ya Yesu Kristo.
Mkate wa juu ushibishao
Ni chakula chetu kweli
Ndani ya Yesu tumepewa
Uzima unaodumu.
Pali pa kikombe kikali
Ulichomunywesha, Mungu
Mwokozi mwema na mupole
Ametupa cha wokovu.
Kwa sauti ya malaika
Tukinyakuliwa juu
Tutamuimbia sifa zake
Tutamuona siku nzuri !
Yesu sadaka ya Mungu
Ulishuka duniani
Ukafunga ile shimo
Itutengayo naye.
Ukavaa mwili wa mutu
Ukateswa kabisa ;
Kwa Kuokoa kiumbe
Ukapata uchungu.
Ni wewe hekima yetu
Uhai na salama
Kimbilio kwa mateso
Wokovu wa milele.
Ee Mwokozi mwaminifu
Twabaki ndani yako
Hadi uzima milele
Waishi tutaishi.
Kwa kutuokoa, Bwana wa uzima
Alisumbuliwa na kuaibiwa
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Pokea mioyo yetu, mshahara wako
Ulioupewa, kwa mlima kalvari.
Kifo chako Yesu, kikaosha zambi
Ukafunga shimo kwa miguu yetu
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Twakusifu Bwana, ulitupa amani
Heri, ukombozi kwa mateso yako.
Kututajirisha, mwenyewe mbinguni
Ukawa maskini, wewe Mungu mkubwa
Sfa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Pokea mapendo na heshima zetu
Viwe kwako Mungu pasipo mwengine.
Mema ya pendo lako Mchungaji wetu
Unatuandalia meza kila siku
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Wapendwa wako Bwana wanafurahi
Wakionja pendo na matunzo yako.
Kwa amani twafwata uriti wetu
Wewe ni sehemu yetu kwa milele
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Mukombozi Mungu, unayetupenda
Upewe nguvu, ufalme na heshima.
Milele na milele tutakusifu
Pendo lako kubwa na ushindi wako
Sifa kwake Mwana
Sifa kwako Kondoo
Pokea mioyo yetu, mshahara wako
Ulioupewa, kwa mlima kalvari.
Nani atatukuza, nani atatambua,
Pendo lililokushusha toka mbinguni
Kwenda Getsemane,...Golgota ya damu
Pale ulipochomwa mkuki na Mungu.
Siyo wale, Bwana, majeshi wa mbinguni,
Ama vile vyote ambavyo uliumba
Ama urefu wa bahari na mbingu,
Vitakavyotukuza upendo wako.
Yesu ! Pendo lako na neema yako nzuri,
Nani atavikuza ? ni sisi waovu tu
Uliofanya wafalme, makuhani,
Kwa ajili yao ulionja kifo.
Wakombolewa tu, kwa raha takatifu,
Wataimba wema wako na kubariki.
Uliwanunua, Ee Yesu, kwa damu
Watakuwa nawe milele mbinguni.
Twakuona ukiangaika
Ukinywa kikombe kile
Tunakuona ukijitoa
Mtakatifu kwetu waovu.
Kifo chako sadaka safi
Tukitazame daima
Damu yako ilituosha,
Ikatufungulia mbingu.
Pendo lako ni kubwa Kristo
Linagusa mioyo zetu
Ulifilia ulimwengu
Wewe ndiye Mwokozi wetu.
Kama Kondoo ulikufa, Yesu
Kwa zambi zetu, Mukombozi wetu
Pendo gani ? ni pendo la ajabu
Kwa kutuokoa, Yesu ukafa.
Kwa ule wakati zambi zetu
Zilikuletea azabu kali
Kwa kufa ukavunja minyororo
Ukatuletea neema, raha.
Amen ! Bwana ! Uwezo na sifa
Kwako heshima, hekima, ufalme
Tangu sasa tunasema na wewe :
Ubarikiwe Ee Mukombozi.
MwanaKondoo uliteswa
Ukachukua taabu yetu
Na ukatufanya kwa Baba
Wafalme na makuhani
Pamoja tunakuheshimu
Twakusifu na kukuinua
Nguvu, ufalme pia kutii
Mioyoni tunakuabudu
Amen ! Amen ! Bwana ! Amen.
Twakuona utukufuni
Ee Mwokozi !
Tukionja ushindi wako
Mwenye nguvu
Milele pamoja na Mungu
Kwa kuume kwa Baba Mungu
Uliyeshuka duniani
Na upole.
Kwa sisi ukawa laana
Ee Mwokozi !
Ukateswa zaidi sana
Ee Mwokozi !
Damu katoka mbavu zako
Ukatuondolea zambi
Kwa kufa kwako tunaishi
Ee Mwokozi.
Tunakungoja toka mbingu
Ee Mwokozi !
Ulisema waja kututwaa
Yesu mweza !
Furaha isiyo na mwisho
Yakutazama sura yako
Na vile yakukufanana
Ee Mwokozi.
Yesu, neema, damu yako
Na musalaba wako
Kungaa kwa uso wako
Vyatupatia haki
Nafsi yetu yapumzika
Ndani yako Mwokozi
Wewe mwanzo na chemchemu
Ya uheri milele.
Katupenda mpaka kufa
Mwokozi wa mapendo
Katushindia shetani
Hadi kwa ngome yake, (x2).
Namna vilikulemea
Pekee kwa saa ya
Kuachwa pia na hofu
Ya zambi zetu nyingi, (x2).
Sasa fujo ya mawimbi
Yaliyokufikia
katuletea pumziko
Ya kazi yako nzuri, (x2).
Kando yako wateule
Wako hapa duniani
Sasa wanaonja raha
Ya nyumba yake Baba, (x2).
Kondoo wa Mungu Kristo akafa
Mutini (x2)
Pazia pale kapasuka
Kwa muti (x2)
Kwa patakatifu sana,
Mbele ya Mungu twafika
Kwako Yesu uliyejitoa
Mutini (x2)
Uliinuliwa toka chini
Mutini (x2)
Ulikunywa kikombe chetu
Mutini (x2)
Kwa pendo kakimaliza
Damu yako ilituosha
Tumeokoka kwa milele
Kwa muti (x2)
Hayani sifa zako kangaa
Mutini (x2)
Yesu uliupata ushindi
Mutini (x2)
Milele upewe nguvu,
Heshima na sifa nyingi
Kwa sababu ulishinda
Mutini (x2)
Nyimbo za mbinguni
Ni nzuri sana
Vinanda na nyimbo
Jaeni mbingu
Kwa nafasi kubwa,
ule wimbo mpya
Daima waanza
Kando ya Kondoo.
Kwa kiti cha enzi
Tutakuona
Ukivikwa taji
Za kila aina
Na mikono yako
Inaonyesha
Ginsi uliteswa
Kwa musalaba
Neema ya milele!
Uliye chinjwa
Ukajitolea,
Kamwanga damu
Kwa patakatifu,
Uheshimiwe
Mungu Baba yako
Aabudiwe.
Nyimbo za mbinguni
Ni nzuri sana
Vinanda na nyimbo,
Vyajaa mbingu
Heshima na nguvu,
Kuzo milele
Kwa Mungu mushindi,
Na Kondoo wake.
Mwana wa Mungu, wa ajabu
Waonekana usoni
Upendo muzuri wa Baba
Hata sifa zake nyingi
Washika dunia mkononi
Uliitosha utupuni
Vyote vinaimba Hekima,
Na kuzo lako Muweza.
Mbele ya Baba kifuani
Wamupendeza daima
Mupo mumoja uwezoni
Mupo mumoja pendoni
Ulipenda, siri ya ajabu
Kutoka patakatifu
Kuja dunia yenye zambi
Ili ufe Mwana Kondoo.
Upendo, neema ya ajabu
Twakuona Mutu, Mungu
Kwa sanduku hadi kalvari
Ukifwata njia chungu
Mugeni, ulikataliwa
Hata na walio wako
Ukanywa kikombe kichungu
Shambani mwa Getsemane.
Ukabeba, Mwana Kondoo
Kwa saa za giza mutini
Hukumu ya makosa yetu
Pia gazabu ya Mungu
Ee Bwana tutakutukuza
Milele kule mbinguni,
Na roho zetu zitaimba
Pendo lishindalo kifo.
Yesu rafiki yetu mkubwa
Pendo gani !
Atupenda kushinda ndugu
Pendo gani !
Jamaa, rafiki, wanapita
Heri yaja na kutoweka
Moyo wake tu hauchoke
Pendo gani
Yu uzima wetu milele
Pendo gani!
Na kwa milele tutukuze
Kazi yake !
Kwa damu yake tumeoshwa
Alipotukuta jangwani
Kwa neema akatuokoa
Pendo gani !
Alijitoa kama zabihu
Pendo gani!
Anapenda kutubariki
Pendo gani!
Nafsi yetu imusikie
Kwa amani, kamwe, isiogope
Iishi karibu na Yeye
Kwa upendo.
Kazi ya milele, tutakapo pumzika
Bila mwishowako watakuabudu
Wakitupa taji juu ya miguu yako
Wakistaajabu na watainama, (x2).
Tutautazama uso wa Muabudiwa,
Uzuri wa Mwokozi, Bwana Arusi
Na tutavumbua fumbo isiyopimwa
Ya neema na mapendo bila mpaka, (x2).
Kwako pekee Yesu, kwa nuru yako nzuri
Wewe jua la haki liangazalo
Kanisa litavaakatika utukufu
Nuru
Utaona pekee lile unalotaka !
Tunda kamili la kazi ya msalaba
Utafurahia kazi ya nafsi yako
Mapendo yako Mungu yatatosheka, (x2).
Twaishi kwako, chemchemu njema
Tufurahie nuru yako
Kukuona mbele ya Baba
Yesu, pumziko ya roho yetu.
Mungu alitutolea Yesu
Na kwake akaleta amani
Akapendezwa na uhaki
Deni yetu kweli imelipwa.
Tuna heri, Bwana wema wako
Umetufungulia mbingu
Na mukristo kwa utulivu
Aingia kwani ameokoka.
Kwa nini tusikupende Yesu ?
Uliyejitolea kwetu
Wewe ambaye pendo lako
Laja kila siku mbele yetu.
Watufunza, watufariji
Yesu ukiwa mbinguni
Kwani Roho na neno Lako
Vyabaki na wateule.
Twasikia sauti yako
Kupitia neno Lako
Roho wako hufahamisha
Agusa moyo na macho.
Kumbukumbu La pendo Lako
Lafikiawalio wako
Katika Jangwa watukuzwa
Twaonja mema ya mbingu.
Hilini Neno La uzima,
Kama tunda La Eskoli
Linalotupatia nguvu
Jangwani tulikulapo.
Muda kitambo kazi yake
Itakwisha kwa kundi hii
Tutakapo kuona nuruni
Tutazungumuza nawe.
Yesu, Nguvu, Mwamba wangu
Mwokozi wangu mkuu
Adui hawataweza
Nikilindwa nawe.
Kwa Neema ulinisamehe
Umenipa mbingu
Ninazungukwa na nguvu
Imani yatosha.
Wewe ndiye Mukombozi
Na mwenye upendo
Wewe ni uheri, sifa
Na Mwokozi wangu.
Neno lako ni aminifu
Bwana halipite kamwe
Nafsi yangu iliaminiyo
Haitaogopa tena.
Ninajuwaee wazo nzuri
Miongoni mwa kondoo zako
Hakutapotea yoyote
Mchungaji uliahidi.
Wana wa pendo lako kubwa
Tupokifuani mwako
Hata dunia na kuzimu
Havitatutosha kwako.
Bwana wangu mwema
Uliniponya
Nipo mushahara
Kwa kazi yako
Nilikuwa mnyonge
Sasa ni wako
Neema yako nzuri
Kaniokowa.
Chunga kwa rehema
Nafsi milele
Katika furaha
Na usalama
Unishike mkono,
Nisilegeye
Nichunge daima
Karibu nawe.
Ni ndani ya Mungu
Kwa tumaini lote
Mioyo yapumzika
Uvumilivu wako,
Rehema yako kubwa
Vinanionyesha
Matunzo ya pendo.
Ni kutamu kwangu !
Kuwa wewe ni Baba
Yu nami popote
Waniangazia neema
Wapokea maombi
Unanitazama,
Wanipa imani.
Salama na pendo
Furaha kamilifu
Ni vyangu milele
Naona mbele yangu
Njia nzuri ya raha
Ni ya utukufu
Yaenda mbinguni.
Bwana niongoze
Ukinishika mkono
Linda nyayo zangu
Mungu kwa pendo lako
Nguvu, hekima yako
Vinatuzunguka
Ni msaada wa nguvu.
Nikufikilipo Bwana
Pia neema yako
Moyo wangu wafurahi
Kwani utakuona, (x2).
Hata kama ninachoka
Ninasonga mbele tu
Kama mahali pakavu
Kunakoota miiba, (x2).
Hata adui ni wengi
Kwa kunishambulia
Kwa mitego ya hatari
Wanizunguka sana, (x2).
Ninaweza kila siku
Kufuata njia yako
Na kwa pendo lako kubwa
Kuonja lifaalo, (x2).
Bwana, pumziko na Mwamba
Wokovu, haki yangu
Wanikaribia mimi
Wanipendeza mimi, (x2).
Yesu, Mukombozi wangu
Nijaze uhodari
Wezesha mtumishi wako
Akuwe mwaminifu, (x2).
Hadi siku wateule
Washindi ndani yako
Wakivaa kanzu nyeupe
Watakuona kuzoni, (x2).
Tumutazamie Yesu,
Bado kitambo Mwokozi
Atarudi toka mbingu,
Katika kungoja kwa heri
Nafsi zetu ziwe tayari
Tuwe macho, tusilale
Wakristo, Mwokozi aja.
Kamwe sitapungukiwa
Kwani Bwana ni Mchungaji
Ninaishi chini ya gongo
La asiyebadilika
Kweli Yesu ulinitia
Miongoni mwa kondoo zako.
Ulinipa salama yako
Najua ulinipenda
Nikipita katika moto
Najua sitaungua
Macho yako ni juu yangu
Ongoza yangu juu yako.
Bwana nikukaribiapo
Sioni woga yeyote
Neema yako ni mwamba mkubwa
Kimbilio haki kwangu
Ulinishika mkononi
Shetani hata nitosha.
Tufurahi wakristo, (x2) ;
Bado kitambo Yesu,
Ndani mwetu atatukuzwa
Bwana utarudia, (x2)
Tutakutana nawe
Na tutaishi ushindi.
Siku gani tutaona
Kanana ya mbinguni ?
Juu ya mbingu mwasikia ?
kristo anatuita.
Na tutaishi naye,
zoruba itakoma
Tutaimba kwa milele
wimbo wa salama.
{Heri kamilifu, Uheri, uheri
Heri kamilifu, Pumziko ni Bwana
Kanisa litakapokusanyika mbinguni
Litaimba bila mwisho :
Sifa kwake Kondoo.}
Wateule wataona,
utukufu wa Kristo
Wakiwa wamefufuka,
watamshuhudia
Wakisifu ushindi,
kazi ya musalaba
Pamoja kando ya kiti,
tutampa naziri.
Kama kule juu mbinguni,
mwenye zambi akitubu,
Malaika kwa umoja,
wabariki Bwana
Itakuwa furaha,
wakati kundi lake
Litakapo kombolewa,
nakushinda vyote.
Kanana ni fasi nzuri,
Ni inchi ya ahadi
Tukikusanywa na Mungu,
kwa upendo wake
Tutaimba milele
wimbo wa kufurahi
Utasikika mbinguni,
Milele daima.
Siku hiyo ya milele,
itaangaa asubui
Sote katika umoja
Na mapendo pia
Na tutasema tena
Na yule Muabudiwa :
Mwana Kondoo astahili
nguvu na mamlaka
{Heri kamilifu, uheri, uheri} etc.
Niwapo na fasi mbinguni
Hapa chini nina amani ya roho
Mbali ya mawimbi na zoruba
Niwezapo pumzisha kichwa
Kifuani mwa Mwokozi
Juu nyumbani mwa Baba yangu
Ndani yako Yesu nina vyote
Vyote vya pali patakatifu
Bwana, uso wako, nuru yangu
Wanipa sifa na pendo.
Tunaweza kukufuata
Njiani mwako Yesu
Ulimopenda kuishi
Ukiwa mgeni kwetu
Ulikuwa pekee yako
Ukitenda mema tu
Katika njia hii nzuri
Yako mtu mkamilifu.
Hiyo njia yafungua
Mema,
Mungu mwenyewe atambua
Humo utakatifu
Hivi kwa neema yako
Twaweza kukufuata
Kwani ulituokoa.
Wabarikiwa wako.
Mwili wetu ukiteswa
Sikitiko na taabu
Tunapoonja uchungu
Tukufuatapo, Yesu
Juu yako twatazamia
Katika uzaifu
Utakatifu wako.
Njia hii yaishia
Inchini penye sifa
Palipo uso wa Mungu
Na wa Mutu mushindi
Tukiwa wakamilifu
Kuzoni tutaabudu
Yesu tutakufanana
Tutashibishwa nawe.
Jangwani nifuatamo njia yangu
Kuelekea inchi ya kuishi,
Kusiwe kizuizo hata kazi
Kwani mbingu ni uriti wangu.
Mwokozi ni Kiongozi, tumaini
Nichunge na hatari ya siku.
Uniangazie kwa usiku
Unichunge pendoni mwako.
Kila asubui mapendo yako
Yanitumia kila siku mukate.
Jioni ninapolala salama
Wewe unahusika na kesho.
Mwamba wangu ! Maji
Yatiririka kuniondolea kiu
Kwa Roho wako unichunge
Moyo wangu usinungunike.
Hivi sasa mwisho wa njia yangu
Utaniletea pumuziko ;
ushuhuda hakika wa Bwana
Unanikinga na mawimbi.
Inchi yangu, ee inchi ya ahadi
Moyo wangu sasa wakusalimu
Katika raha tele takatifu
Jina lako Mungu lisifiwe.
Kuokolewa kutoka inchi
Ya utumwa, zambi, giza
Tunatarajia uriti
Tukiongozwa na Roho.
Huko hatutalia tena
Kazi, kiu vile njaa
Hakuna hatari, kilio
Ni amani, uheri tu.
Milele pamoja na Kundi
Upendoni kwa furaha
Tutakusifu kwa milele
Kondoo uliyetufia.
Kujeni wapendwa, tuchote kwa furaha
Amani na neema kwa chemchemu
Tutangaze mema, tuinue upendo
Wa Mwokozi anayetuponya, (x2).
Tutakutukuza, Bwana nyimboni mwetu
Tunaojua mapendo yako
Ulitutendea mambo mazuri
Tutakubariki siku zote, (x2).
Twakuabudu Yesu, Mwokozi wa mapendo
Uliyetuokoa kwa damu
Twaimba upendo wako hapa duniani
Mbinguni tutauimba daima, (x2).
Furaha gani, tunyakuliwapo
Yesu akirudi
Na milele Kanisa litakwenda
Mbali ya dunia, (x2).
Wakati mzuri, Kristo atatuleta
Karibu ya Baba
Tutakapotukuzwa mbele yake
Kristo atatuingiza, (x2).
Kutasikika kule juu mbinguni
Nyimbo za heri tu
Wote watatangaza neema yake
Pendo la Mwokozi, (x2).
Shuka mbinguni, tunakuhitaji
Twakupenda, kuja
Tangu zamani tunakungojea
Bwana arusi njoo, (x2).
Wateulewako
Katikavita,
Wakutapohapa
Unyongemwingi,
Mbinguniwabebwa
Moyonimwako
Eekuhaniwetu
Mukubwasana.
Ukijaanawema
Napendopia
Hautamsahau
Mukombolewa
Niwewemsaada
Katikavita
Unatutetea
Mungu Mtetezi.
Kwakilauchafu
Niwewepekee
Utusafishaye
Miguukwamaji
Wasema : mwamini
« Niigemimi
Mufanokamili
Mtumishimwema. »
Tundalaushindi,
Wakombolewa,
Watakuwanawe
Kuzonimwako
Nyumbanimwa Baba
Usonimwake
Tumepewakazi :
Nipendolako.
Neema gani Bwana, kuitwa ndugu zako
Na kuwa na amani, tukikungojea
Ulitufungua kutoka shida zetu
Haki yetu, pendo lako, (x2).
Ni wewe uliyetusafisha kwa damu
Na moiyoni mwetu, ukaleta amani,
Yesu, mkate wa juu, chakula cha mbinguni,
Kwako tupo wa milele, (x2).
Mshindi wa shetani na dunia
Bwana Yesu amefufuka
Na Kwa woga wa
Siku nzuri inafwata
Hakuna woga, ziki tena
Enyi taifa teule,
Pamoja na furaha tele
Tuimbe Yesu amefufuka.
Siku yaja ya raha kubwa
Mwili huu utainuka
Umepandwa muharibifu
Utafufuka kuzoni
Miili yetu ya uzaifu
Itakapobadilishwa
Yesu utaifananisha
Na mwili wako wa kuzo .
Tayari kwa uhai wako
Yesu tumefufuliwa
Ndani yako, kwa neema yako
Tumepanda juu mbinguni
Kwa kungojea siku yako
Itakayoonekana
Tukikutegemea wewe
Tunapiga vita nzuri.
Ni kutamu kupenda Mungu Baba
Kumwendea sawa, bila woga
Kufanya kazi hapa duniani
Tukiongozwa na Roho wa Bwana.
Ni kutamu kupata kwa saa zote
Rafiki mpendwa na msaidizi
Kuwa huru kuingia mbele yako
Kupata msaada hatarini !
Ni kutamu kuwaza neema yako,
Kwa Uzaifu na ulegevu
Na kusema : Alitwaa fasi yetu
Akateswa kama Mwana Kondoo
Ni kutamu kuona sifa zako,
Bwana Yesu, na watakatifu,
Kungoja kwa salama siku yako
Ya ushindi bei ya imani !
Siku gani mbele ya kiti chako,
Watakatifu wametukuzwa,
Kila moja akivaa taji yake
Wataziweka kwa miguu yako !
Haki yako kamili,
Ee Mwokozi ni uzuri
Na kuonekana kwa heshima
Kwa aliye kombolewa.
Uliturehemu kabisa
Na tumepewa zawadi
Pia uhakika imara
Twangojea siku kubwa.
Kwetu taifa kamilifu,
Hakuna tena hukumu
Hakuna pia woga kwetu !
Mungu alitusamehe.
Yesu wewe ni haki yetu,
Wasema : naja upesi
Kanisa lote lifurahi,
Kukuona Mukombozi !
Ndugu sote tusimame
Tuna Mwalimu hapa
Bwana arusi yu aja
Kristo ataonekana, (x2).
Karibu atatawala
Pamoja na kanisa
Punde atalivika taji
La sifa ya ahadi, (x2).
Usiogope kundi ndogo
Wewe mpendwa wa Baba
Msalaba wa Mwana Kondoo
Uwe bendera yako, (x2).
Dunia ikikuchukia
Chuki yake ni kuzo,
Pendo, tumaini, imani
Vitakupa ushindi, (x2).
Sifa kwa Yesu Mwokozi
Tunamutumainia
Heri anayemuabudu
Ndani ya moyo wake, (x2).
Tunainua, ee Baba mpenzi
Kwako mioyo yetu na mikono
Na maombi twakutolea
Pendoni safi na ukweli
Kama waabudu wa kweli.
Mbele yako twajisikia
Kama tumepewa Mwana wako
Wana wa neema yako ya mbingu
Tuna fasi rohoni mwako
Kama Yesu na rafiki.
Tumependwa jinsi tulivyo
Unyonge watusumbuwa sisi,
Na kuita mapendo yako.
kwa Roho tuliyeahidiwa,
Uzaifuni twabariki.
Tukipiga hivi mwendo huu,
Twaelekea kwako, Ee Yesu,
Ndani yako hazina yetu,
Maji ya chem.chemu ya mbinguni
Na mkate wa wateule.
Tangu asubui, mioyo yakubariki.
Mchana na usiku, tu mkononi mwako
kwa wana wako, wema wako haukomi
Tena watupenda bila hata kuchoka.
Tunaomba kwako neema ya ajabu:
Utulishe leo na mkate wa mbingu;
Tunajingojea kwa musaada wako;
Daima watufunika na mkono wako.
Roho wako Mungu atufundishe njia,
Kwa neno lako takatifu mioyoni!
Tukitiwa nguvu naye hakuna woga,
Na tupo washindi pamoja na Kristo.
Tupo wasafiri, wageni duniani,
Moyo wetu unahaja ya mbinguni.
Ni mbinguni mwako, Mungu na baba wetu
Tutakapoingia kwa pendo lako.
Utuchunge katika safari salama,
Hadi siku ya heri bila magumu,
Tutaonja pamoja uheri muzuri,
Wakati Yesu atakapo tupumuzisha.
Sifaidiki wala kupoteza
Jangwani humu sina chaguo :
Hakuna pori hata jani bichi,
Hakuna maji yakuninywesha.
Jangwani hakuna kimbilio,
Wala pumziko hata kidogo,
Kwa nini mimi nisimame bure
Ninapokaribia kufika?
Jangwani mimi ninajua njia :
Njia ya pendo, neema na imani,
Nitakayoifwata bila shaka,
Kwani Mwokozi aliipasua.
Njia ya nguvu ijaayo heri,
Ambamo yote ni salama tu ;
Iniongozayo toka duniani,
Ilinifike kwa Baba Mungu.
Bila tamaa, bila kazi na woga,
Umenifundisha kukaa pale,
Nitaonja, pale patakatifu
Pumziko karibu nawedaima.
Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi
Pendo la Mwokozi
Neema yake amini
Siku zote ni mpya
Inaangaa sana
{Yeye mkubwa na muzuri
Tumsifu Bwana, (x2).}
Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi
Pendo la Mwokozi
Kiti cha neema
Fasi ya hakika
Kwa mioyo yetu
{Yeye mkubwa na muzuri} etc.
Tuimbe, tuimbe katika wimbo safi
Pendo la Mwokozi
Yesu utukufuni
Ni ushindi wetu
Na heri yetu
{Yeye mkubwa na muzuri} etc.
Sifa, uwezo na nguvu
Heshima kwake Mungu
Upendo na shukurani
Kwake Yesu Mwokozi.
Mwokozi ulivikwa miiba
Damu yakokamwangwa
Hata gazabu ya Mungu
Na Ikakulemea.
Kwako ee Yesu mateso
Kilio, kifo, kuachwa
Na kwa sisi ukombozi
Wokovu, usamehe.
Sifa, uwezo na nguvu
Heshima kwake Mungu
Upendo na shukurani
Kwake Yesu Mwokozi.